Kiungo Mohammed Issa 'Banka' amesema kiwango kilichoonyeshwa na Abdulaziz Makame kwenye mchezo dhidi ya Zesco, ni dalili njema kuwa fundi huyo ameanza kurejea kwenye ubora wake
Makame aliyetua Yanga kutoka Mafunzo Fc ya Zanzibar, hakuwa amepata nafasi kwenye kikosi cha kwanza kabla ya mchezo dhidi ya Zesco
Makame alicheza namba sita, alikuwa kikwazo kwa Zesco
Banka, Makame na Fei Toto walianza pamoja huku Banka akipangwa namba saba
"Kwa mimi ninayemfahamu Makame kile kiwango alichokionyesha mechi na Zesco bado, licha ya mashabiki kusifia kiwango chake, hapo ndiyo kwanza gari limeweka subiria kumuona akionyesha kiwango zaidi ya hicho ambacho amekionyesha," Banka alimsifu kiungo huyo ambaye wameitwa pamoja na Fei Toto kwenye kikosi cha Stars
"Namba sita ndiyo nafasi yake anayoicheza, awali alikuwa hapati nafasi ya kucheza na mimi nilikuwa nikicheza namba sita kutokana na yeye kukosa mechi fitnesi ambayo tayari imeanza kurudi taratibu, hivyo Wanayanga wasubirie mengi kwake"