Hivi ni kweli Yanga imeshindwa kumalizana na Chikupe?

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
21 Sep 2019
Hivi ni kweli Yanga imeshindwa kumalizana na Chikupe?

Beki Andrew Vicent Chikupe bado hajajiunga na kambi ya kikosi cha Yanga kinachojiandaa na mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Zesco United

Mchezo huo utapigwa Jumamosi ijayo, Septemba 28 kwenye uwanja wa Levy Mwanawasa nchini Zambia

Chikupe hajafanya mazoezi kabisa na klabu ya Yanga tangu kuanza kwa msimu huu ikielezwa anashinikiza kulipwa madai yake ya fedha za miaka ya nyuma

Mara kadhaa uongozi wa Yanga umetoa taarifa ya kuwepo kwa majadiliano na mchezaji huyo lakini mpaka sasa hakuonekani kupatikana muafaka

Inatia mashaka kuwa suala lake huenda likaishia kama ilivyokuwa kwa mlinda lango Beno Kakolanya aliyejiunga na Simba baada ya mkataba wake na Yanga kuvunjwa

Kujirudia kwa matukio haya hakuleti picha nzuri kwa taasisi ya Yanga

Busara inafaa itumike ili kumaliza sintofahamu hii ili kuilinda taswira ya Yanga

Kama Chikupe ana madai kweli basi inafaa uongozi wa Yanga ukamalizana nae ili aweze kujiunga na wenzake

Ukizungumzia wachezaji walioipigania Yanga wakati wa 'hali ngumu', Chikupe ni mmoja wao

Ni mchezaji mwenye nidhamu, hakuwahi kugoma wakati wote ambao Yanga ilikuwa ikipita katika nyakati ngumu

Ni jambo jema kuona hata kocha Mwinyi Zahera ametambua mchango wake na kuutaka uongozi wa Yanga umlipe stahiki zake ili aweze kurejea kikosini

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’