Majeraha yamuweka Balama nje wiki mbili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Sep 2019
Majeraha yamuweka Balama nje wiki mbili

Kiungo mshambuliaji Mapinduzi Balama atakuwa nje kwa wiki mbili kuuguza majeraha ya paja aliyopata kwenye mchezo dhidi ya Zesco United

Balama aliyecheza namba mbili kwenye mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, aliumia kwenye dakika ya 75 na nafasi yake kuchukuliwa na Ally Ally

Kocha Mwinyi Zahera huenda akalazimika kumtumia Juma Abdul kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Zesco nchini Zambia kwani Paulo Godfrey 'Boxer' nae bado hajarejea kikosini

Daktari wa Yanga Dk Edward Bavu amethibitisha kuwa Balama atakuwa nje kwa muda huo baada ya kufanyiwa vipimo na kubaini ukubwa wa jeraha lake

"Balama hatakuwa sehemu ya kikosi chetu kitakachorudiana na Zesco katika mchezo wa marudiano, ni baada ya kumfanyia vipimo na kuonekana amepata maumivu makubwa kwenye paja lake.

"Alipata majeraha hayo tulipocheza na Zesco katika mchezo wa kwanza wa hapa nyumbani ambao alishindwa kumalizia mechi hiyo baada ya kusikia maumivu kabla ya kuomba atolewe nje.

"Hivyo baada ya kufanyiwa vipimo akaonekana amepata majeraha makubwa, atatakiwa akae nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili zaidi lakini nafanya jitihada za kuhakikisha anapona haraka ili arejee uwanjani," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
14h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’