Baada ya kutoka jela ya soka kwa kuruhusiwa kuichezea Yanga, wikiendi iliyopita kiungo Pius Buswita alipiga 'mpira mwingi' katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.
Buswita, aliyesajiliwa kutoka Mbao FC ameahidi kulipa fadhila kwa kuifungia timu yake mabao na kuisaidia kutwaa ubingwa wa VPL kwa msimu wa nne mfululizo.
"Niko fiti kuhakikisha nafanya kila liwezekanalo ili kuipa Yanga ushindi na hilo litawezekana kutokana na sapoti kubwa ninayoipata kutoka kwa uongozi wa timu," amefunguka Buswita.
"Nawashukuru viongozi wa Yanga kwa kunipigania hadi kupata nafasi hii ya kucheza, baada ya awali kufungiwa kwa mwaka mmoja".
Buswita aliibuka kuwa nyota wa mchezo ikiwa ni mechi yake ya kwanza tangu atolewe kifungoni.

ADVERTISE HERE