Mshambuliaji wa Yanga, Issa Bigirimana leo ameanza mazoezi ya uwanjani na kikosi cha Yanga baada ya kuwa nje kwa muda mrefu akikosa karibu mechi zote za mashindano.
Katika mazoezi ya leo asubuhi kwenye Viwanja vya Chuo cha Polisi Kurasini, Bigirimana alianza kwa kwa kupewa maelekezo ya mazoezi anayotakiwa kuanza na kocha wake Mwinyi Zahera.
Mshambuliaji huyo mwenye asili wa Burundi, mwenye uraia wa Rwanda alikimbia kwa dakika 10, akizungunguka uwanja huku baada ya muda huo akichezea mpira akipiga danadana.
Mazoezi hayo aliyafanya kwa dakika 45 kabla ya kutakiwa kupumzika kwa muda akiwangalia wenzake walijifua ndani ya uwanja.
Endapo atafanikiwa kuwa sawa huenda akaiongezea nguvu timu yake katika mchezo ujao dhidi ya Zesco.
Mapema Zahera alisema kukosekana kwa mshambuliaji huyo kumepunguza upana wa kuchagua washambuliaji wake kutokana na ubora wa Bigirimana.
Bigirimana alitua Yanga akitokea klabu ya APR akisaini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria