Makame amvuruga Lwandamina

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Sep 2019
Makame amvuruga Lwandamina

Kocha Mkuu wa Zesco United George Lwandamina amekiri kuwa kiungo mkabaji wa Yanga Abdulaziz Makame 'Bui' ndiye aliyewavuruga mipango yao jijini Dar es salaam akishukuru kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Yanga kwenye mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa

Katika mchezo huo, Makame alicheza sehemu ya kiungo pamoja na 'nduguze' kutoka visiwani Zanzibar Feisal Salum 'Fei Toto' na Mohammed Issa 'Banka'

Mkufunzi huyo wa zamani wa Yanga amesema alivutiwa na aina ya uchezaji wa Bui mara kwa mara akihusika kukata mawasiliano baina safu ya kiungo na washambuliaji wa Zesco

Kiwango alichoonyesha Bui kwenye mchezo huo, kimemuweka kwenye nafasi nzuri ya kujihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza

Kocha Mwinyi Zahera alisema Makame alitimiza vyema majukumu aliyompa katika mchezo huo

Makame ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Sudan kusaka tiketi ya kutinga fainali za CHAN

Wachezaji wengine wa Yanga walioitwa ni pamoja na mlinda lango Metacha Mnata, Kelvin Yondani, Mohammed Issa na Feisal Salum

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
39m ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
10h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
15h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
19h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
20h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
20h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’