Kama ilivyokuwa Botswana, Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela anatarajiwa kuongoza msafara wa maafisa wa timu hiyo nchini Zambia kuweka mambo sawa kabla ya kikosi kuwasili mwanzoni mwa wiki ijayo
Yanga inatarajiwa kwenda Zambia Septemba 23 kuweka kambi ya siku tano kuelekea mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Zesco ambao utapigwa Septemba 28
Mwakalebela ndiye aliyeongoza msafara wa Yanga Botswana, akihakikisha timu inakuwa na mazingira mazuri ya maandalizi wakati wote waliokuwa nchini humo
Kwa sasa Yanga inaendelea kujifua jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo huo ambao matokeo ya ushindi yatawapa nafasi ya kutinga hatua ya makundi
ADVERTISE HERE