Zoezi la kumwaga kifusi kwenye uwanja wa Kaunda unaomilikiwa na klabu ya Yanga liko katika hatua za mwisho na wakati wowote matengenezo ya sehemu ya kuchezea 'pitch' yataanza
Zoezi la kifusi limechukua muda mrefu kutokana na mazingira ya eneo la Jangwani ambapo makandarasi wa Uwanja huo walipendekeza kujazwa kifusi kingi kitakachohimili wingi wa maji wakati wa mvua
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Dismas Ten amesema wanatarajia kuanza matengenezo ya sehemu ya kuchezea ambapo kutokana na ukubwa wa eneo, kutakuwa na viwanja viwili, kimoja cha nyasi bandia na kingine cha nyasi asili
Ten amesema malengo yao ni kutengeneza uwanja ambao pamoja na kuutumia kwa ajili ya mazoezi, watautumia katika baadhi ya michezo
Tangu uongozi mpya wa Yanga ulipoingia madarakani, kumekuwa na michakato mingi hapo Jangwani
Ukarabati wa uwanja, ukarabaji wa Jengo na wakati wowote kampuni ya GSM itaanza ujenzi wa duka kubwa la klabu ambalo litakuwa likiuza bidhaa mbalimbali za Yanga
Baada ya kushinda zabuni ya usambazaji wa jezi za Yanga, kampuni ya GSM pia itahusika kukarabati jengo pamoja na duka hilo
Pamoja na kukarabati uwanja wa Kaunda, Yanga ina eneo kubwa zaidi (ekari saba) Kigamboni walilopewa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda
Kulingana na Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla, Kigamboni Yanga itajenga viwanja viwili pia, kimoja cha Kimataifa na kingine cha kawaida
Pia watajenga Academy ya klabu ya Yanga