Mchezo wa kwanza kati ya Tanzania dhidi ya Sudan wa kuwania tiketi ya kufuzu fainali za michuano ya CHAN kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani, utapigwa Jumapili Septemba 22 2019, saa moja usiku
Mchezo huo ambao Tanzania itakuwa mwenyeji, utapigwa uwanja wa Taifa huku mchezo wa marudiano ukitarajiwa kupigwa Oktoba 19 nchini Uganda
Sudan imechagua kuhamishia mchezo wake wa nyumbani Uganda kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama nchini mwao
Timu itakayoibuka na ushindi wa jumla, itajihakikishia tiketi ya kucheza fainali za CHAN ambazo zitafanyika mwakani huko Cameroon
ADVERTISE HERE