Nahodha msaidizi wa Yanga Thabani Kamusoko alilazimika kutumia viatu maalumu kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Mtibwa Sugar kutokana na hofu ya kutonesha majeraha yake.
Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kuhusu 'pitch', sehemu ya kuchezea ya uwanja wa Uhuru kuwa ni ngumu sana na inachangia kwa kiasi kikubwa majeruhi ya mara kwa mara ya wachezaji.
Bahati mbaya kwa kuwa Yanga haina uwanja wake, imekuwa ikiutumia uwanja huo kwa mazoezi hivyo kuongeza hatari ya wachezaji wake kupatwa na majeruhi.
Kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar Kamusoko alilazimika kutumia viatu vyenye meno mafupi, viatu ambavyo huvitumia wakati wa mazoezi.
Ni jambo mchakato wa ukarabati wa uwanja wa Kaunda unaendelea, ukikamilika utapunguza hofu hiyo kwa wachezaji wanapotumia uwanja wa Uhuru.

ADVERTISE HERE