Wakati Yanga ikiendelea na maandalizi ya mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Zesco, rekodi ya timu hiyo ugenini inawapa matumaini mashabiki wake kuwa watafanya vizuri Zambia
Tangu mwaka 2014 Yanga imepoteza michezo miwili tu ugenini kwenye michuano ya ligi ya mabingwa
Al Ahly ndio time pekee iliyoifunga Yanga; Mwaka 2014 ikishinda kwa mikwaju ya penati baada ya matokeo ya 1-0, matokeo kama hayo iliyapata Yanga kwenye mchezo wa kwanza uwanja wa Taifa. Mwaka 2016 ikashinda tena 2-1
Ni takwimu ambazo zinadhihirisha uimara wa Yanga itapocheza ugenini
Juzi kocha wa Zesco United George Lwandamina alikiri kuifahamu rekodi hiyo, yeye akiwa mmoja wa waliofanikisha wakati akiinoa Yanga
"Nafahamu Yanga imekuwa na rekodi ya kufanya vizuri inapokuwa ugenini lakini pia Zesco haijawahi kupoteza mchezo uwanja wa nyumbani tangu mwaka 2014. Hivyo mchezo wa marudiano utakuwa na ushindani wa aina yake," alisema
Yanga inaendelea kujifua uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam na itaelekea Zambia mwanzoni mwa wiki ijayo ambapo itaweka kambi ta siku saba nchini humo