Kikosi cha mabingwa wa kihistoria Tanzania, Yanga kinakabiliwa na mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Zesco United
Mchezo huo utapigwa nchini Zambia Jumamosi ya Septemba 28
Mpango mkakati wa Yanga ni kushinda ugenini ili waweze kutinga hatua ya makundi
Licha ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa juzi katika uwanja wa Taifa, Yanga bado ina nafasi kama itashinda au kupata sare ya kuanzia mabao mawili
Sare ya bao 1-1 itapeleka mchezo kwenye matuta
Katika kuhakikisha wachezaji wanazoea mazingira ya Zambia, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka nchini Jumatatu ijayo, Septemba 23
Yanga wataondoka nchini baada ya kumaliza majukumu ya ligi kuu, wakikabiliwana mchezo dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa Jumamosi, Septemba 21 katika uwanja wa Sokoine
Katika raundi ya awali kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Township Rollers, Yanga walikwenda Botswana mapema na kuweka kambi nchini humo
Kambi hiyo iliwasaidia kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na kufanikiwa kutinga raundi ya kwanza