Mshambuliaji tegemeo wa klabu ya Yanga Donald Ngoma atakuwa tayari kurudi dimbani katika mchezo wa mzunguuko wa sita ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Kagera Sugar Oktoba 14.
Ngoma alishindwa kufanya mazoezi na kikosi cha Yanga juzi akikabiliwa na maumivu ya misuli.
Daktari wa Yanga Dk Edward Bavu amesema wamebaini tatizo la mshambuliaji huyo na tayari ameanza matibabu yatakayodumu kwa siku saba.
Akizungumza kitaalamu, Dk Bavu amesema misuli ya paja la Ngoma mguu wa kulia, ilivutika sana hivyo kumsababishia maumivu makali.
Awali ilidhaniwa mchezaji huyo amechanika nyama za paja.
Sasa ni dhahiri mchezaji huyo hayuko hatarini kukosa michezo ijayo ya timu yake.

ADVERTISE HERE