Yanga bado wapo sana Kimataifa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Sep 2019
Yanga bado wapo sana Kimataifa

Wakati mashabiki wa Simba wakiendelea kusherehekea sare ya bao 1-1 waliyopata Yanga dhidi ya Zesco United jana, mabingwa hao wa kihistoria bado wataendelea kuwatesa watani zao hata ikitokea wameondoshwa michuano ya ligi ya mabingwa

Mashabiki wa Simba wanaiombea Yanga 'dua baya' ili iondoshwe kwenye michuano ya Kimataifa baada ya timu yao kushindwa kupenya hatua ya awali wakitolewa na UD Songo

Baada ya kufanikiwa kutinga raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa, Yanga walijihakikishia tiketi mbili

Ya kwanza ni kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo kama watapata matokeo ya ushindi Zambia

Lakini ya pili, kama wakitolewa na Zesco, watahamia kwenye  michuano ya kombe la shirikisho

Utaratibu wa CAF uko hivi;

Timu 16 ambazo zitashinda raundi ya kwanza ya ligi ya mabingwa, zitatinga hatua ya makundi

Nyingine 16 ambazo zitatolewa raundi hiyo, zitaungana na tmu 16 zilizofuzu raundi ya pili ya michuano ya kombe la Shirikisho

Zitacheza raundi moja ya kusaka timu za kutinga makundi kombe la Shirikisho

Msimu wa 2015/16 Yanga walitolewa na Zanaco raundi ya kwanza ya ligi ya mabingwa, wakapangwa na Sagrada Esperanca ya Angola hatua ya mtoano wa kufuzu makundi kombe la Shirikisho na wakatinga hatua hiyo kwa ushindi wa mabao 2-1

Wakarudia tena msimu wa 2017/18 kwa kutinga makundi kombe la Shirikisho kwa kuindosha Wolayta Dicha ya Ethiopia kwa kuifunga mabao 2-1 baada ya kutolewa na Township Rollers kwenye ligi ya mabingwa

Hivyo hata kama watakosa nafasi ya kutinga makundi ligi ya mabingwa, wataendelea kubaki anga za Kimataifa wakisaka nafasi nyingine ya kutinga makundi kombe la Shirikisho

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
6h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’