Ni utamaduni wa wachezaji kutoshangilia wanapozifunga timu zao za zamani wanapokutana nazo kwenye mchezo wa kwanza
Jambo hilo halikutokea kwa Thabani Kamusoko ambaye leo aliifungia ZESCO bao la kusawazisha kwenye dakika ya mwisho kabisa ya mchezo
Licha ya kucheza Yanga kwa miaka minne, wakati mwingine akiwa nahodha, Kamusoko alishangilia bao lake kama haijui Yanga tena akitumia aina ya ushangiliaji ya Heritier Makambo aliyotumia msimu uliopita
Ni dhahiri mkongwe huyo alikuwa akionyesha hasira zake baada ya kutemwa na kocha Mwinyi Zahera
Kamusoko ni miongoni mwa wachezaji ambao walitamani kuendelea kubaki Yanga lakini nafasi hiyo hakuipata na badala yake akajiunga na ZESCO United
Mkongwe huyo ambaye kuishi kwake Tanzania kumemfanya aifahamu lugha ya kiswahili kwa ufasaha, anaonekana kurejesha makali yake