Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera leo alivalia mavazi yake ya siku zote pensi na Tshirt kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa dhidi ya ZESCO United, mchezo ukimalizika kwa sare ya bao 1-1
Mashabiki waliojitokeza dimba la Taifa, wengi walivalia mavazi hayo kumuunga mkono Mcongomani huyo aliyekumbana na adhabu ya Bodi ya Ligi akielezwa mavazi yake sio 'nadhifu'
Kanuni hiyo imetungwa kulenga michezo ya ndani tu kwani haipo CAF wala FIFA


ADVERTISE HERE