Sibomana, Balinya na Sadney wapewa kazi ya kuimaliza ZESCO United

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Sep 2019
Sibomana, Balinya na Sadney wapewa kazi ya kuimaliza ZESCO United

Washambuliaji Juma Balinya, Sadney Urikhob na Patrick Sibomana kwa mara nyingine, watakiongoza kikosi cha Yanga kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa dhidi ya ZESCO United utakaopigwa kesho Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa

Balinya na Sadney walikuwa jijini Mwanza kwenye kambi ya maandalizi kuelekea mchezo huo wakati Sibomana alirejea kwao Rwanda kutimiza majukumu ya timu ya Taifa

Hata hivyo Sibomana 'PS' amerudi akiwa 'fit' na hivyo kuongeza matumaini kuelekea mchezo huo

Moja ya changamoto zilizoikabili Yanga kwenye michezo ya hivi karibuni ni uhaba wa mabao

Hata hivyo kocha Mwinyi Zahera amesema changamoto hiyo imefanyiwa kazi

Katika michezo miwili ya kirafiki ambayo Yanga ilicheza jijini Mwanza, walifunga mabao manne na kuruhusu bao moja

Licha ya David Molinga ambaye alifunga mabao matatu kwenye ziara hiyo kukosekana, Zahera amesema ana imani na washambuliaji hao watatu

"Balinya ameonyesha mabadiliko, nlizungumza nae na kumjenga kisaikolojia, nadhani sasa atafunga mabao mengi" alisema Zahera

"Huyu ni mshambuliaji aliyekuwa mfungaji bora ligi kuu ya Uganda akifunga mabao 21 msimu uliopita, sina wasiwasi na uwezo wake"

"Sadney pia alikuwa na matatizo ya kukosa kujiamini. Kambi ya Mwanza imetusaidia kufanyia kazi mapungufu yote"

"Mashabiki waje kwa wingi uwanjani, tumejiandaa kushinda mchezo huo"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’