TAARIFA
Mwenyekiti wa Yanga Dr. Mshindo Msola, kwa niaba ya Baraza la Wadhamini, Kamati ya Utendaji, Wanachama na Washabiki wa Yanga pia kwa niaba ya wadhamini wa klabu yetu @sportpesatz, gsmtanzania @taifagas anapenda kupokea shukrani za dhati zilizotolewa na Mh. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa leo Bungeni jijini Dodoma.
Pia, Mwenyekiti wa Yanga anatoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Jemedari na Mwananchi Namba Moja Dkt. Joseph Pombe Magufuli kwa sera safi za michezo na ushirikiano inaopata klabu yetu kupitia Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.
Klabu ya Yanga inatumia fursa hii kuwaomba Watanzania wote wajitokeze kwa wingi kesho Uwanja wa Taifa saa tano asubuhi ili kuisapoti timu yetu na kuhakikisha bendera ya Taifa letu Tanzania inapeperushwa ipasavyo na kwa ushindi mnono.
Ahsante sana na Shukrani Kwa Serikali na wadau wote..