Aliyekuwa kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania Emmanuel Amunike amelishtaki Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa Shirikisho la mchezo huo Duniani (FIFA) kwa kutokulipwa sitahiki zake
Amunike aliyeisaidia Tanzania kufuzu kwa michuano ya Afcon 2019 baada ya kusubiri kwa miaka 39, mkataba wake ulivunjwa baada ya Tanzania kuishia hatua ya makundi
Inaelezwa alikuwa na madai ya malimbizo ya mishahara pamoja na gharama za kuvunja mkataba wake
Amunike hakudumu Stars, akiiongoza timu hiyo katika michezo 10 pekee
Katika michezo hiyo, Stars ilishinda michezo miwili, sare miwili na kufungwa michezo sita
ADVERTISE HERE