Wapinzani wa Yanga kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa, ZESCO United wanatarajiwa kuwasili nchini leo kuelekea mchezo utakaopigwa Jumamosi, Septemba 14 2019 kwenye uwanja wa Taifa
Kikosi cha timu hiyo kinatarajiwa kuja nchini na msafara utakaojumuisha wachezaji 19
Miongoni mwa wachezaji hao ni Thabani Kamusoko ambaye amejiunga na timu hiyo usajili wa msimu huu baada ya mkataba wake na Yanga kumalizika
Kamusoko ameitumikia Yanga kwa misimu minne
Kocha Mkuu wa timu hiyo George Lwandamina, anakuja nchini kwa mara ya kwanza kuchuana na Yanga, timu aliyoifundisha kwa msimu mmoja na nusu kabla ya kutimkia ZESCO United
Wakati ZESCO ikitua nchini leo, kikosi cha Yanga ambacho kiliweka kambi jini Mwanza kujiandaa na mchezo huo, kinatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam leo
