Lazima tuwamalize ZESCO uwanja wa Taifa - Zahera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Sep 2019
Lazima tuwamalize ZESCO uwanja wa Taifa - Zahera

Zikiwa zimebaki siku tatu kabla ya mchezo wao wa awali wa raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco ya Zambia, Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, ameweka wazi kuwa mechi hiyo itakuwa ngumu, lakini ni lazima kazi waimalizie Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kabla ya mchezo wa jana wa kirafiki dhidi ya Toto African ya Mwanza, Zahera alisema wamejipanga 'kumalizia kazi' Uwanja wa Taifa kwa kuwa anaamini mchezo wa marudiano nchini Zambia utakuwa mgumu zaidi.

"Unajua lazima tupambane sana kwenye mchezo wa nyumbani, ushindi mzuri utatupa nafuu kuelekea kwenye mechi ya marudiano na utatupa nafasi ya kujipanga zaidi na kujua nini tunatakiwa kwenda kufanya ugenini," alisema Zahera.

Alisema hana hofu na timu yake na yapo mambo aliyoyafanyia kazi ambayo anaamini yatawasaidia kwenye mchezo huo utakaochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa.

"Kila mchezo una mipango yake, tumemaliza mchezo wa kwanza dhidi ya Township Rollers, hatutacheza kwa namna tulivyocheza... mchezo huu una mipango yake na tunaendelea kuifanyia kazi hatua za mwisho," aliongeza kusema Zahera.

Zahera, amesema kikubwa anataka kuona wachezaji wake wote wanakuwa kwenye afya nzuri mpaka siku ya mchezo ili kumpa wigo mpana kwa kuona wachezaji wa kuwatumia kutokana na mbinu atakazotumia kwenye mechi hiyo.

Katika hatua nyingine, winga wa timu hiyo, Issa Bigirimana anaendelea kupata nafuu kutokana na maumivu ya paja yanayomkabili.

Nyota huyo wa Yanga hakuweza kuungana na wenzake kwenye kambi mkoani Mwanza kutokana na maumivu hayo.

Baada ya mchezo huo wa Jumapili, Yanga itarudiana na wapinzani wao hao wiki mbili baadaye nchini Zambia.

Nipashe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’