Ni dhahiri kiungo mshambuliaji Mapinduzi Balama anaweza akacheza namba mbili kwenye mechi ya ligi ya mabingwa dhidi ya ZESCO United itakayopigwa Jumamosi Septemba 14 kwenye uwanja wa Taifa
Beki Paulo Godfrey 'Boxer' huenda asiwe tayari kwa mchezo huo kutokana na majeraha aliyopata kwenye mchezo dhidi ya Township Rollers
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera alimchezesha Balama namba mbili katika michezo ya kirafiki dhidi ya Toto Africans na Pamba Fc, alifanya vizuri
Yanga imekuwa ikikabiliwa na changamoto upande wa kulia pale Boxer anapokosekana
Ukiondoa Juma Abdul ambaye hivi karibuni alipata msiba wa kufiwa na mama yake, Yanga haina mchezaji mwingine mwenye uwezo wa kucheza namba hiyo
Kwa nyakati tofauti Zahera aliwajaribu Ally Ally, Cleofas Sospeter na Mustafa Suleyman ambao kwa asili ni walinzi wa kati
Aina ya uchezaji wao hauinufaishi Yanga wakicheza pembeni kwa kuwa hawana uzoefu na nafasi hiyo
Katika michezo miwili aliyocheza, Balama ameonyesha utofauti mkubwa, akiwa mahiri katika kupeleka mashambulizi