Molinga aomba sapoti ya mashabiki Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Sep 2019
Molinga aomba sapoti ya mashabiki Yanga

Mshambuliaji wa Yanga David Molinga amewataka mashabiki wa timu hiyo waendelee kumuunga mkono akiahidi kuwapa furaha msimu huu

Molinga amepata na mafanikio kwenye ziara ya Yanga mkoani Mwanza akifunga mabao matatu kati ya manne yaliyofungwa na timu yake katika michezo dhidi ya Pamba na Toto Africans

"Nilichelewa kufika, nilikuta wenzangu wamefanya kazi nzuri, nami nimekuwa nikijituma ili niweze kuwa bora zaidi," alisema Molinga baada ya mchezo dhidi ya Toto Africans jana

"Nawaambia mashabiki waendelee kuniunga mkono, msimu huu ninawaahidi kuwapa furaha"

Jana Molinga alifunga mabao mawili kati ya matatu kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Toto Africans

Akizungumzia kiwango cha mshambuliaji huyo, mchezaji wa zamani wa Yanga na timu ya Taifa Sekilojo Chambua, amesema Molinga ameonyesha kuwa na kiu ya kutaka kufunga kila mara

"Molinga ameonyesha kuwa na kiu ya kutaka kufunga kila mara, hilo ni jambo jema. Mabao haya aliyofunga bila shaka yatamuongezea kujiamini, " alisema Chambua

"Nafikiri atapata mafanikio Yanga kama ataendelea hivi ingawa bado hayuko sawa kimwili, anahitaji kupunguza uzito"

Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera alimpa Mcongomani huyo program ya kupunguza uzito ambapo alisema amepungua kilo 10 katika kipindi cha siku 40

Zahera alisema Molinga alikuja nchini akiwa na kilo 84 lakini sasa ana kilo 74

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
38m ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
4h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
23h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’