Kiungo wa Yanga Issa Bigirimana yuko jijini Dar es salaam akiendelea na matibabu ya majeraha ya nyama za paja
Bigirimana alibaki Dar wakati wenzie wakiweka kambi ya kujiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa jijini Mwanza
Kiungo huyo aliyekuwa akitabiriwa kufanya mambo makubwa Yanga, ameanza maisha yake ndani ya Yanga vibaya kutokana na kuandamwa na majeraha hayo aliyopata wakati mabingwa hao wa kihistoria walipokuwa wameweka kambi mkoani Morogoro
Juzi alikuwepo uwanja wa Taifa kushuhudia mchezo kati ya Tanzania dhidi ya Burundi
ADVERTISE HERE