Pensi ndio vazi rasmi la Septemba 14

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Sep 2019
Pensi ndio vazi rasmi la Septemba 14

Jumamosi ya Septemba 14 ni siku muhimu sana kwa Wanayanga ambapo timu yao itashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Zesco United katika mchezo wa kwanza wa kusaka nafasi ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa

Ni mchezo ambao kila Mwanayanga anajua matokeo ya ushindi ni lazima, kujitokeza kwa wingi kuujaza uwanja wa Taifa ni jambo la lazima pia

Lakini siku hiyo pia Wanayanga wamepanga kupaza sauti zao kwa utaratibu maalum kupinga adhabu ya mavazi aliyopewa kocha wao Mwinyi Zahera

Zahera aliadhibiwa na Bodi ya Ligi akitakiwa kulipa faini ya Tsh 500,000/- baada ya kuvaa 'pensi' kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting

Wanayanga wameazimia kuonyesha umoja wao kwa kumuunga mkono Zahera ambapo siku hiyo 'pensi' litakuwa vazi rasmi kwa viongozi na mashabiki

Ni kuonyesha kutokubaliana na kanuni hiyo ya mavazi ambayo kimsingi inaonekana imemlenga zaidi Zahera kwani yeye ndio hutumia zaidi mavazi hayo na ndiye kocha wa kwanza kukumbana na adhabu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
2h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
20h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’