Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema bado washambuliaji wake wanashindwa kutumia vyema nafasi wanazotengeneza
Akizungumza baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Pamba Fc ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1, Zahera alisema walistahili kuibuka na ushindi mnono hata hivyo wamekosa nafasi nyingi huku akimpongeza mlinda lango wa Pamba Fc kwa kazi nzuri aliyofanya
Zahera amesema bado wachezaji wake wanakosa kujiamini wawapo langoni kwa timu pinzani
Hata hivyo amesema hali hiyo ni ya muda tu, wakati utafika watafunga mabao mengi
"Hatuwezi kucheza mechi 10 tukose magoli kama tunavyokosa hapa. Tulikosa mabao mechi dhidi ya Ruvu Shooting, leo pia tumekosa"
"Hali hii haitaendelea kwa mechi zote, wakati utafika watafunga"
Amfunga kazi Molinga
Katika hatua nyingine, Zahera amesema bao alilofunga David Molinga leo, litazidi kumuongezea kujiamini
Zahera amefichua kuwa amempa Molinga program ya kupunguza uzito sasa akiwa amepungua kilo nne
Amesema tatizo lake hakuwa amecheza mechi nyingi za kimashindano, michezo hii ya kirafiki inaendelea kumuimarisha