Molinga afuta 'nuksi', afunga bao Yanga ikitoka 1-1 na Pamba Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Sep 2019
Molinga afuta 'nuksi', afunga bao Yanga ikitoka 1-1 na Pamba Fc

Mchezo wa kirafiki kati ya Pamba dhidi ya Yanga uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba, umamalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1

Pamba walipata bao la kuongoza kwenye dakika ya 30 kupitia kwa Saada Kipanga

Mcongomani David Molinga 'Falcao' leo amefungua akaunti ya mabao kunako klabu ya Yanga baada ya kuisawazishia kwenye dakika ya 90

Awali Molinga alifunga bao ambalo lilikataliwa na mwamuzi kwa kuwa alikuwa ameotea

Tangu mwanzo wa mchezo huo, Molinga alionekana kuwa na shauku ya kupachika bao, hata hivyo majaribio yake mengi yaliokolewa na mlinda lango wa Pamba FC

Pamba ilimaliza mchezo huo ikiwa na wachezaji 10 uwanjani baada ya kiungo Hamis Thabit kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga ngumi Feisal Salum pale wachezaji hao walipotofautiana

Pamba walionyesha upinzani mkali kwa Yanga kwenye kipindi cha kwanza lakini Yanga ikauchukua mchezo kwenye kipindi cha pili

Washambuliaji walikosa umakini katika kumalizia nafasi nyingi zilizotengenezwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’