Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma huenda akingia kwenye orodha ya majeruhi baada ya leo kusindwa kufanya mazoezi kufuatia maumivu makali ya misuli.
Ngoma alishindwa kumaliza mchezo dhidi ya Mtibwa juzi ambapo alitolewa kwenye dakika ya 80 na nafasi yake kuchukuliwa na Juma Mahadhi.
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema mchezaji huyo atafanyiwa vipimo kubaini madhara aliyopata na daktari wa Yanga, Dk Edward Bavu amesema zoezi hilo litafanyika ndani ya masaa 24.
Ngoma ameifungia Yanga mabao mawili katika michezo mitano akiwa sawa na Ibrahim Ajib mwenye idadi kama hiyo ya mabao.
Ngoma hajakuwa katika kiwango bora msimu huu pengine ni athari za majeruhi yaliyomuweka nje kwa muda mrefu msimu uliopita.
Amekuwa akionekana kuugulia maumivu mara kadhaa kwenye michezo aliyocheza msimu huu.

ADVERTISE HERE