Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema adhabu ya kufungiwa mechi tatu aliyopewa na Bodi ya ligi haiwezi kuiathiri timu yake kwa kuwa kocha Noel Mwandlla yupo
Zahera ambaye yuko Mwanza akikinoa kikosi chake kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya ZESCO United, ameongeza kuwa adhabu hiyo aliyopewa sio haki kwani kosa lake ni kulalamika baada ya maombi ya kutaka mechi dhidi ya Ruvu Shooting isogezwe mbele kukataliwa
Mbali na kufungiwa mechi tatu, alilimwa faini ya sh 500,00 kwa madai ya kutovaa mavazi nadhifu wakati walipocheza dhidi ya Ruvu Shooting na kuipa Yanga onyo kwa kushindwa kuhakikisha kocha wao anakuwa nadhifu.
Zahera amesema Bodi imemtafutia sababu tu, kwani kama kuomba mechi kusogezwa mbele, mbona kuna timu ilikuwa na viporo hadi 16 msimu uliopita, na iliomba mechi zake kusogezwa mbele, na ilikubaliwa.
Hatahivyo, amesema kukosekama kwake katika benchi la ufundi, hakutaharibu kitu, kwani anaimani na msaidizi wake Noel Mwandila kuisaidia timu kufanya vizuri katika mechi hizo atakazokosa
"Msimu uliopita, niliposafiri katika majukumu ya timu ya Taifa (Congo), Mwandila aliiongoza timu kupata matokeo kwa kushinda mechi nne katika michezo mitano ya Ligi Kuu, tulipoteza mchezo mmoja tu dhidi ya Lipuli, hivyo sina wasiwasi," amesema
Zahera atakosa mechi tatu dhidi ya Tanzania Prisons, Mbeya City na Polisi Tanzania