Yanga inaelekea jijini Mwanza kuweka kambi ya maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya ZESCO United
Mchezo huo utapigwa Septemba 14 kwenye uwanja wa Taifa
Ikiwa Mwanza, kocha Mwinyi Zahera amependekeza wacheze mechi mbili za kirafiki ambazo hazitahusisha timu za ligi kuu
Mchezo wa kwanza utakuwa Jumamosi, Septemba 07 dhidi ya Gwambina Fc inayoshiriki ligi daraja la kwanza
Mchezo huo utapigwa Wilayani Misungwi na utakuwa mbashara kupitia Azam Sport 2
Jumanne, Septemba 10 Yanga itarejea Mwanza kuumana na Pamba Fc kabla ya kuanza safari ya kurudi Dar tayari kwa mchezo dhidi ya ZESCO United
ADVERTISE HERE