Kamati ya Bodi ya ligi imempiga faini kocha wa Yanga Mwinyi Zahera kwa kuvaa walichoeleza mavazi yasiyo nadhifu na ya heshima katika mechi dhidi ya Ruvu Shooting, kinyume na Kanuni ya 14(2m) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo
Wakati Zahera akiadhibiwa kwa mavazi hayo, kocha wa Ruvu Shooting ambaye hakukumbana na adhabu yoyote, mavazi aliyokuwa amevaa hayakuwa na tofauti na yale ya Zahera (pensi na t-sheti)

Pengine TFF inapaswa kufafanua yepi ni mavazi ya heshima na yepi sio kwani mazingira kama haya yanaweza kuthibitisha kile kinachosemwa kuwa sheria hii alitungiwa mtu mmoja
ADVERTISE HERE