Simba imechupa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Vodacom baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Stand United.
Kabla ya matokeo hayo Simba ilikuwa nafasi ya sita lakini ushindi umeifanya iongoze ligi kwa tofauti ya mabao kwani ina alama 11 sawa na Mtibwa Sugar sambamba na Azam FC.
Yanga inashika nafasi ya sita ikiwa na alama tisa sawa na Prisons iliyo nafasi ya tano huku Singida United ikiwa na alama 10 kwenye nafasi ya nne.
Mchuano kwenye nafasi za juu bado ni mkali kwani tofauti ya alama kati ya Simba iliyo kileleni na Yanga iliyo nafasi ya sita ni alama mbili tu.
Michezo miwili ya Yanga inayofuta itapigwa ugenini ambapo kwanza itakwenda Kagera kuchuana na Kagera Sugar Oktoba 14 kisha kuifuata Stand United Oktoba 22.
Yanga inahitaji ushindi kwenye michezo hiyo ambayo itakuwa migumu sana. Ugumu wa michezo hiyo unatokana na nafasi zilizopo Stand United na Kagera Sugar.
Kagera Sugar iko mkiani ikiwa na alama mbili wakati Stand United iko kwenye nafasi ya 15 ikiwa na alama tatu.
Kwa msimamo kamili nenda kwenye ukurasa wa MSIMAMO.
Baada ya michezo hiyo Yanga itarudi Dar kwenye dimba la Uhuru kuivaa Simba Oktoba 28.
Mchezo huu pia unaweza kuhamishiwa kwenye dimba la CCM Kirumba kama maombi ya Yanga yatakubaliwa na TFF.

ADVERTISE HERE