Yanga inatarajiwa kuelekea jijini Mwanza kuweka kambi ya maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya ZESCO United ambao utapigwa Septemba 14 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Awali ilielezwa kuwa ikiwa jijini Mwanza Yanga itacheza mechi mbili za kirafiki
Hata hivyo kwa ushauri wa kocha Mwinyi Zahera, huenda Yanga itacheza mechi moja tu dhidi ya Pamba Fc
Imeelezwa kocha Zahera amekataa timu yake kucheza mechi ngumu akihofia wachezaji wake kuumia kuelekea mchezo dhidi ya ZESCO
Ni kawaida kwa Mbao Fc kukamia michezo wanayokutana na Yanga kwenye uwanja wa CCM Kirumba, jambo hilo limempa hofu Zahera na kuamua timu yake ni vyema ikacheza na timu zisizoshiriki ligi kuu
Mchezo dhidi ya Pamba Fc utapigwa siku ya Jumanne, Septemba 10 katika uwanja wa CCM Kirumba