Kikosi cha Yanga kesho Jumatano, Septemba 04 2019 kinatarajiwa kuelekea Mwanza kuweka kambi ya maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya ZESCO United
Mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa Taifa, Septemba 14 2019
Ikiwa jijini Mwanza, Yanga inatarajiwa kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Pamba Fc na Mbao Fc
Imeelezwa kambi hiyo imeandaliwa na wapenzi, wanachama na mashabiki wa Yanga wa jijini Mwanza
Uongozi wa Yanga hautatumia gharama yoyote kwani hata timu itakapokuwa Mwanza itakuwa chini ya Wanachama hao
Aidha mapato yatakayopatikana kwenye michezo ya kirafiki, asilimia 85 yataingia kwenye mfuko wa Yanga
ADVERTISE HERE