Chikupe amegoma kuripoti kambini Yanga, hadi alipwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Sep 2019
Chikupe amegoma kuripoti kambini Yanga, hadi alipwe

Licha ya uongozi wa Yanga kumsihi beki Andrew Vicent aripoti kambini kuendelea na mazoezi ya maandalizi ya mchezo dhidi ya ZESCO, amekataa

Kumekuwa na majadiliano baina ya uongozi wa Yanga na mchezaji huyo ambaye anadai fedha zinazofikia Tsh Milioni 18 yakiwa ni madai ya mishahara ya nyuma na fedha za usajili

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema juzi katika kikao cha Kamati ya Utendaji, suala lake lilijadiliwa na kufikia muafaka alipwe mara moja fedha zitakapopatikana, lakini aripoti kambini kuanza mazoezi

Mwakalebela amesema sio yeye pekee anayeidai Yanga, wachezaji wengi wakiwemo wengine ambao wamehama, wana madai lakini amewahakikishia watalipwa

Misimu miwili iliyopita, Yanga ilikubwa na ukata uliopelekea kuwa na malimbikizo ya mishahara ya wachezaji na fedha za usajili

Mwakalebela amesema wamekuwa wakimaliza madai hayo taratibu huku wakihakikisha hawaongezi madeni kutoka kwa wachezaji waliopo sasa

Beki Kelvin Yondani na Juma Abdul ni miongoni mwa wachezaji ambao waliweka mgomo kushinikiza walipwe, wao walikubali kupokea sehemu ya malipo yao na kurejea mazoezini

Chikupe ametaka kulipwa fedha zake zote ndio arudi mazoezini

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’