Yaliyojiri Mkutano wa viongozi wa Matawi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Sep 2019
Yaliyojiri Mkutano wa viongozi wa Matawi Yanga

Dondoo za mkutano wa Jana Baina ya Matawi na Mwenyekiti wa klabu Dr Msolla -

Mkutano ulikuwa na lengo moja kuhamasisha amani na umoja ndani ya Yanga kuelekea mechi na Zesco pamoja na mechi 37 za ligi kuu zilizobaki

Matawi yasaidiane pamoja na klabu kuhakikisha Yanga inashinda mechi zake zote zilizobaki za ligi kuu pamoja na mechi ya Kimataifa

Katika kuleta umoja wa klabu tuondoe makundi makundi yote yaliyokuwepo Wakati wa uchaguzi na Sasa Yanga iwe moja atakayechochea makundi kupelekwa Kamati ya Nidhamu kushugulikiwa

Matawi yametakiwa yafanye chaguzi kufikia December na katika kuhakikisha Hilo litasimamiwa Mwenyekiti yupo mbioni kuunda Kamati ya Matawi na wanachama itakayokua inasimamia Masuala ya Matawi na wanachama kwa ujumla.

Kwa muda wa miezi minne Kamati mpya ya Utendaji imekwisha ingia mikataba zaidi ya minne kuhakikisha Yanga inakua vyema kiuchumi

Jengo la klabu ya Yanga Sasa ukarabati utaanza muda sio mrefu na utafanywa na Kampuni ya GSM kwa kuwa moja ya masharti katika tenda ya jezi iwaliyopewa limo pia sharti la kukarabati Jengo ili Sasa kupunguza matumizi ya kukaa hotelini

Ukarabati utahusisha pia sehemu ya mazoezi ya viungo Gym pamoja na bwawa la kuogelea lililopo katika Jengo

Mpaka Sasa Yanga Ina mkataba na Sportpesa ambao mwaka huu watatoa Bilioni Moja na milioni 94

Uongozi umefanikiwa kupata mikataba na Taifa Gas toka kwa Rostam ambao watato milioni 300

Lakini pia ushirikiano na Mh Rostam bado upo ndie aliyetoa milioni 60 kuvunja mkataba wa Kindoki na pesa za kumleta Molinga Yanga

Mkataba na GSM wa Kwanza ni ule wa jezi ambao klabu unapata TSH 1300 kwa kila jezi itakayouzwa na lengo ni kuhakikisha jezi milioni 1 zinauzwa ili klabu ipate Bilioni Moja na milioni 300, pia mkataba unahusisha ukarabati wa Jengo la Yanga

Mkataba wa pili na GSM unahusisha magodoro ya GSM mkataba huu una thamani ya milioni 150

Klabu ipo mbioni kuongeza mdhamini mwingine toka Kampuni ya Vinywaji atakayetoa pesa Kama ilivyo Sportpesa na pia kukarabati pitch ya uwanja wa Kaunda uwe wa kisasa kutumika katika mazoezi ndio maana zoezi la kuweka kifusi linaendelea kwa kasi

Ishu ya Zahera kupewa mechi tatu

Si kweli kwamba Mwl Zahera amepewa mechi tatu, bali juzi Kulikua na kikao cha Kamati ya Utendaji na kocha aliitwa atambulishwe rasmi kwa wajumbe na pia ashauri mikakati ya kuelekea mechi na Zesco na kiujumla Uongozi una imani na kocha na wanaushirikiano mzuri hivyo habari kuwa amepewa mechi tatu, zimetungwa

Kuhusu sectretaliet tayari mchakato wa kuwapata Katibu na Wakurugenzi wa idara mbalimbali Kama Fedha ,Masoko,Ufundi na Mashindano umeshakamilika na wiki hii watapewa ofa ya mikataba tayari kwa kuanza kazi

Kuweka kambi Mwanza

Timu itaelekea Mwanza kwa maandalizi ya mechi na Zesco itaondoka Tarehe 4 Mpaka tarehe 11 Itakua Mwanza

Ikiwa Mwanza kutakua na Kubwa Kuliko tamasha la kuichangia Yanga lililoandaliwa na wanayanga wenyewe wa Mwanza

Wana Mwanza wamelipia kila kitu kuhusu safari hiyo hivyo klabu haitahusika na gharama yeyote na itafaidika katika mechi 2 za kirafiki kwa kupata 85% ya gate collection.

Gazeti la Yanga liko mbioni na litalejea mda sio mrefu

Mwisho wanayanga wote wametakiwa wawe wamoja, wale waliokua nje ya timu na sasa wamerudi Ni juhudi za Mwenyekiti kuhakikisha Yanga yote inakuwa moja hivyo hakuna haja ya kujenga visas. Kila mwanachama ametakiwa asiache kuhudhuria mechi yetu na Zesco.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’