Mwanachama maarufu wa Yanga Mzee Ibrahim Akilimali amewaomba Watanzania kumchangia ili aweze kulipa deni analodaiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
Mzee Akilimali ambaye ni kiongozi wa Baraza la Wazee la Yanga, amesema anahitaji michango kutoka kwa wadau ili kulipa deni hilo baada ya kufanyiwa operesheni ndogo tumboni
Mzee Akilimali amesema anadaiwa fedha kiasi cha Tsh 369,000/
"Hali yangu si mbaya kwa sasa, naendelea vizuri lakini nadaiwa shilingi 369,000 na mpaka sasa sijalipa chochote, naomba kama wadau wataguswa na kuumwa kwangu wanisaidie walau hata kidogo," amesema
"Inabidi nianze kulipa walau kidogokidogo maana sasa nikienda hospitali kwa ratiba niliyopewa na daktari nitakuwa sifanyiwi huduma maana sijalipa chochote, hata wao wamenitaka nilipe la sivyo sitahudumiwa"
Namba ya simu ya Mzee Akilimali ni 0658668819 na jina ni IBRAHIM OMARY AKILIMALI