ZESCO lazima 'wafe' uwanja wa Taifa, Septemba 14

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Sep 2019
ZESCO lazima 'wafe' uwanja wa Taifa, Septemba 14

Mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza michuano ya ligi ya mabingwa kati ya Yanga dhidi ya ZESCO United, umepangwa kupigwa Septemba 14 kwenye uwanja wa Taifa, saa kumi kamili jioni

Ni mchezo ambao Yanga inahitaji kupata ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa mara ya pili

Kwa Tanzania, Yanga ndio timu ya kwanza kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa, ikifanya hivyo mwaka 1998 wakati huo michuano hiyo ikishirikisha timu nane tu

Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa kihistoria Mwinyi Zahera amesema wanayo kila sababu ya kushinda mchezo huo unaopigwa ardhi ya nyumbani

Lakini muhimu zaidi amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani siku hiyo kuujaza uwanja kama walivyofanya siku ya kilele cha wiki ya Mwananchi

Juzi Zahera aliwaambia waandishi wa habari kuwa kama Simba iliweza kushinda michezo yake ya ligi ya mabingwa iliyopigwa uwanja wa Taifa, kwa nini Yanga nayo isishinde?

Yanga inajifua kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini jijini Dar es salaam, lakini inatarajiwa kuelekea jijini Mwanza kuweka kambi maalum kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo

Ikiwa Mwanza Yanga inatarajiwa kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Pamba Fc na Mbao FC

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
5h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’