Aiana ya uchezaji wa mshambuliaji mpya wa Yanga David Molinga, umemuibua Amissi Tambwe aliyemtabiria kuwa atafanya mambo makubwa
Tambwe amesema alimuona Molinga kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting na kubaini ni mchezaji mwenye vitu vingi na kumkumbusha miaka minne iliyopita wakati Yanga ilipomsajili Donald Ngoma
"Jamaa anajua ila sema tu inavyoonekana alikuwa hajacheza soka muda mrefu kama alivyokuwa Heritier Makambo wakati anakuja Yanga, wengi walimuona hafai ila baada ya muda akawa staa," Tambwe amenukuliwa na Championi
"Kwa namna nilivyomuona anaonekana ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kumiliki mpira pia kutengeneza nafasi sasa hivi ni kati ya vitu ambavyo mshambuliaji aliyekamilika anatakiwa kuwanavyo"
"Zile pasi alizokuwa akiwatengenezea wenzake kwa kifua na kichwa hazina tofauti kabisa na zile alizokuwa akinitengezea Donald Ngoma wakati tulipokuwa wote Yanga, kama ningekuwepo basi ningefunga mabao mengi kwa pasi zake"
Juzi kocha Mwinyi Zahera alisema Molinga hakuwa amecheza mechi za kiushindani kwa muda mrefu ndio maana ameanza taratibu kwenye kikosi cha Yanga
Aidha Zahera alisema alimpa program maalum ya mazoezi ambayo mpaka sasa imemfanya apungue uzito
Anaamini Molinga atawanyamazisha wote wanaomkosoa sasa kama ilivyokuwa kwa Heritier Makambo ambaye mwanzoni alionekana kama 'galasa'