Mshambuliaji wa zamani wa Yanga Amissi Tambwe amekamilisha usajili wa kujiunga na Fanja ya Oman
Tambwe aliyeitumikia Yanga kwa misimu minne, anajiunga na timu hiyo akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake katika klabu ya Yanga
Klabu ya Fanja pia anacheza beki wa zamani wa Yanga Mbuyi Twitte
Tambwe ameacha historia katika klabu ya Yanga kutokana na umahiri wake wa kuzifumania nyavu
Alitua Tanzania mwaka 2013 akisajiliwa na klabu ya Simba ambay aliitumikia kwa msimu mmoja kabla ya kujiunga na Yanga
ADVERTISE HERE