Je ni kweli washambuliaji Yanga hawana ubora?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Aug 2019
Je ni kweli washambuliaji Yanga hawana ubora?

Yanga imeanza kwa kusuasua msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom juzi ikikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Ruvu Shooting

Kipigo hicho kimekoleza mjadala kuhusu uimara wa kikosi cha Yanga hasa safu yake ya ushambuliaji

Licha ya kufuzu raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa, wapo wanaoamini kuwa Yanga imepita kwa bahati na matumaini ya kusonga mbele ni madogo kutokana na changamoto ya uhaba wa mabao

Wapo waliokwenda mbali zaidi kwa kusema washambuliaji waliosajiliwa na kocha Mwinyi Zahera hawana uwezo wa kuipa mafanikio Yanga, bora walioondoka

Lakini je, ni kweli kuwa washambuliaji waliosajiliwa hawana uwezo? 

Hebu tuangalie, wachezaji wapya wanaounda safu ya ushambuliaji ya Yanga ni pamoja na Sadney Urikhob, Juma Balinya, Maybin Kalengo, David Molinga na Patrick Sibomana

Balinya alikuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Uganda msimu uliopita akifunga mabao 24, hakuna shaka juu ya uwezo wake wa kuzifumania nyavu

Molinga alifunga mabao 11 ligi kuu ya Congo msimu uliopita, alizidiwa mabao matano tu na mfungaji bora wa ligi hiyo

Aidha Sadney ambaye ni mshambuliaji aliyecheza timu nyingi, rekodi zinaonyesha amefunga mabao angalau nane kwa kila timu aliyocheza

Sibomana yeye kwa asili ni winga, kazi yake tayari imejitangaza Yanga

Kalengo ni mshambuliaji anayeendelea kukomaa, huyu anapaswa apewe muda zaidi

Lakini hakuna shaka, Balinya,  Molinga na Sadney, kinachowasumbua sasa ni ugeni wao

Naamini wakati utafika washambuliaji hao wataanza kufunga

Tofauti na watani zao Simba, Yanga ni kama imeanza kusuka upya timu yake

Zaidi ya robo tatu ya wachezaji wa kikosi cha kwanza ni wapya

Hapa uvumilivu wa mashabiki unahitajika, hakuna shaka, nyota waliosajiliwa Yanga wengi wana uwezo mkubwa

Japo ni kweli wapo wachezaji ambao hawakufikia matarajio ya wengi akiwemo kiungo mshambuliaji Issa Bigirimana

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’