Huwezi kuitoa Yanga kwenye mbio za Ubingwa baada ya michezo mitano

Admin By Admin
β€’
1 Oct 2017
Huwezi kuitoa Yanga kwenye mbio za Ubingwa baada ya michezo mitano
Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu ina ushindani wa hali ya juu. Timu zote zimejipanga. Utalithibitisha hilo kwa kutizama takwimu za matokeo na msimamo wa ligi.

Mzunguuko wa tano unatarajiwa kukamilika leo kwa Stand United kumenyana na Simba mkoani Shinyanga.

Kabla ya mchezo huo Simba iko nafasi ya sita ikiwa na alama nane lakini ikishinda inakwenda kuongoza ligi kwa tofauti ya mabao tu kwani itakuwa na alama sawa na timu za Mtibwa Sugar na Azam FC.

Katika michezo ya mzunguuko wa tano iliyopigwa jana Jumamosi michezo sita hakuna timu iliyoibuka na ushindi. Ni mchezo mmoja tu wa Ndanda dhidi ya Lipuli ambapo Ndanda ilishinda 2-1.

Tofauti ya alama kati ya timu inayoongoza ligi na timu ya nane ni nne tu. Ndanda FC iko nafasi ya nane ikiwa na alama saba wakati Mtibwa Sugar inaongoza ikiwa na alama 11.

Yanga iko nafasi ya tano ikiwa na alama 9, alama mbili nyuma ya Mtibwa Sugar inayongoza ligi.

Hata hivyo Yanga inaweza kurudi chini kwa nafasi moja kama Simba itashinda au hata kutoka sare dhidi ya Stand United.

Bado ni mapema sana kuiondoa Yanga kwenye mbio za ubingwa tena ikiwa imeachwa alama mbili na anayeongoza ligi.

Huu hautakuwa msimu wa kwanza kwa Yanga kutokea nyuma na kutwaa ubingwa. Kuna kipindi hali ilikuwa mbaya zaidi msimu uliopita pale ilipoachwa kwa alama tisa na Simba!

Mwisho wa siku ubingwa ulikwenda Jangwani.

Ni kawaida kwa Yanga kuanza taratibu na kumaliza kwa nguvu. Na jambo la kutia moyo ni kuwa Yanga imekuwa ikiimarika kwenye kila mchezo.

Katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar kama si uimara wa mlinda lango wa timu hiyo Benedict Tinoco Yanga ingeweza kufunga mabao si chini ya matatu.

Ilicheza vizuri pengine kuliko michezo yote ya ligi iliyocheza mpaka sasa. Wachezaji walionekana kuwa na ari, na nafasi za kufunga zilitengenezwa nyingi.

Bado hakuna kilichoharibika, wale wanaomlaumu kocha kwa matokeo sidhani kama wanamtendea haki. Kwa mtizamo wangu naona ametimiza wajibu wake wa kufundisha jukumu la kutumbukiza mpira wavuni sio lake.

Na juhudi za wachezaji tumeziona katika mchezo uliopita, mapungufu machache yaliyojitokeza ni ya mchezaji mmoja mmoja ambayo yamekuwa yakifanyiwa kazi kila baada ya mchezo.

Lwandamina aachwe afanye kazi kwani Yanga bado haijatolewa kwenye mbio za Ubingwa.

Kwa maoni yangu, kwa jinsi ligi ilivyo si jambo jema kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi wakati huu. Kwa sababu wachezaji ni walewale hata akija kocha mwingine hatakuja na wachezaji wengine.

Hata changamoto za nje ya uwanja zinazowakabili wachezaji bado zitakuwa ni zilezile.

Kama washambuliaji wanakosa nafasi za wazi wataendelea kukosa hata aje Guardiola. Kocha anafundisha kabla na baada ya mchezo lakini ndani ya mchezo anatoa maelekezo tu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’