Molinga na nyota wengine Yanga watafanya vizuri - SMG

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Aug 2019
Molinga na nyota wengine Yanga watafanya vizuri - SMG

Siku chache alizokaa na straika mpya wa Yanga, David Molinga, kocha wa timu ya vijana wa Wanajangwani hao, Said Maulid ‘SMG’, amesema mchezaji huyo akipewa muda, atafanya mambo makubwa.

SMG aliachiwa Molinga na wachezaji wengine wiki iliyopita kuwasimamia katika mazoezi, wakati Yanga ilipokuwa Botswana kuvaana na Township Rollers, ukiwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika walioshinda bao 1-0.

Akizungumzia tathmini ya kikosi cha Yanga, SMG amesema hakuna mchezaji mbovu katika kikosi cha timu hiyo , kinachowasumbua watu wengi ni kutokufahamu kuwa wanatakiwa kupata muda wa kutosha wa kuzoeana.

Alisema alibaki akiwafuatilia wachezaji hao, hasa wale wanaoambiwa si wazuri na kubaini viwango vyao ni bora, kinachohitajika ni muda wa kuzoeana.

"Hakuna mchezaji mbaya, tena kama hii michuano ya kimataifa ingechezwa timu zikiwa tayari zipo katika ligi, timu ingekuwa na kasi kubwa zaidi," SMG amenukuliwa na gazeti la Bingwa

"Ujue mchezaji mpya unahitaji muda kidogo wa kuzoeana na wenzako uliowakuta, sasa ukiangalia timu ya Yanga, wachezaji wengi ni wapya na kila mmoja ametoka katika ligi tofauti"

SMG alisema anaamini si Molinga pekee, bali wachezaji wengi wa Yanga watafanya vizuri na kwamba kila mmoja atafurahi kwa sababu watakuwa na mechi nyingi za ligi zitakazowajenga.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’