Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kinatarajiwa kuingia kambini leo kujiwinda na mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu hatua ya makundi kusaka tiketi ya kutinga fainali za kombe la dunia mwaka 2022
Stars itasafiri kwenda nchini Burundi ambapo Septemba 04 itacheza mechi ya kwanza na kisha timu hizo kurudiana jijini Dar es salaam Septemba 08
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidau, alisema maandalizi kwa ajili ya mchezo huo yanaendelea vizuri wakishirikiana na serikali kuhakikisha Taifa Stars inaifunga Burundi.
Aidha, alisema kwa upande wa wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi tayari wamewatumia tiketi zao ili kuja kujiunga na wenzao lengo likiwa ni kuhakikisha wanashinda mechi hiyo na kusonga mbele.
Wachezaji wanne wa Yanga watajiunga na timu hiyo baada ya mchezo wa leo dhidi ya Ruvu Shooting
Nyota hao ni Metacha Mnata, Kelvin Yondani, Abdulaziz Makame na Mohammed Issa 'Banka' ambaye hata hivyo imeelezwa ni majeruhi