Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewaambia wachezaji wake kuwa mechi za ligi kuu ni ngumu kuliko ligi ya mabingwa hivyo wanapaswa kupambana ili kuweza kushinda
Akizungumza kwenye mazoezi ya maandalizi ya mwisho ya kikosi cha Yanga ambayo yamefanyika uwanja wa Uhuru, Zahera amesema wanatarajia kupata upinzani mkali kutoka kwa Ruvu Shooting kesho
"Nimewaambia wachezaji wangu, wanapaswa kupambana zaidi ya walivyofanya Botswana," amesema
"Mchezo dhidi ya Ruvu shooting utakuwa mgumu, wanapaswa kujituma ili waweze kushinda wasije wakabweteka na matokeo ya ushindi ligi ya mabingwa"
"Nimewaambia wachezaji wale waliobakia na wapya kuwa walikuja hapa kwa ajili ya ligi kwani wakati tunawasajili hatukujua kama tutacheza ligi ya mabingwa"
"Hivyo siku ya kesho ndio siku yao muhimu zaidi kudhihirisha uwepo wao kwenye kikosi cha Yanga"
Yanga imeshafanya mazoezi ya mwisho uwanja wa Uhuru kuelekea mchezo huo
Β