Beki wa kimataifa wa Ufaransa, Mamadou Sakho anayechezea Liverpool ya England usiku wa jana alikuwa mgeni maalum wakati wa mechi mahsusi ya klabu ya Taifa Jang'ombe kumuaga beki wake, Abdallah Hajji 'Ninja' anayehamia Yanga.
Ninja aliyesaini mkataba wa miaka miwili mapema mwezi huu kujiunga na Yanga, alicheza kwa dakika 10 tu baada ya kuingia kutokea benchi dakika ya 46 na Taifa Jang'ombe ikachapwa 2-1 na Mlandege.
Na Sakho alikuwepo uwanjani kama mgeni maalum akasalimiana na wachezaji wote, akapiga picha na vikosi vyote kabla ya kwenda jukwaani kushuhudia mchezo huo, mabao ya Mlandege yakifungwa na Abdallah Edi Mundo dakika ya 60 na Razak Khalfan dakika ya 78, wakati la Taifa lilifungwa na Ali Badru dakika ya 30.

ADVERTISE HERE