Baada ya kuwasili usiku wa kuamkia leo, kikosi cha Yanga kimeingia kambini Hotel ya Nefaland kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting
Mchezo huo utapigwa keshokutwa Jumatano, August 28 kwenye uwanja wa Taifa
Kocha Mwinyi Zahera amesema wanahitaji kuanza vyema ligi, wakiwa na malengo ya kutwaa ubingwa msimu huu
Awali Yanga iliomba mchezo dhidi ya Ruvu Shooting usogezwe mbele, hata hivyo Bodi ya ligi ilikataa ombi hilo
Wachezaji watakuwa na mapumziko ya siku moja kabla ya kurejea tena dimbani kuwakabili maafande hao wa Ruvu
ADVERTISE HERE