Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema hawezi kuzungumzia matokeo ya Simba kwa kuwa hakuona mchezo wao
Zahera aliyewasili usiku wa kuamkia leo kutoka Botswana akiwa na kikosi cha Yanga, amesema kwa sasa anachowaza ni mchezo ujao wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting
Kuhusu mchezo dhidi ya ZESCO, Zahera amesema pia huu sio wakati wake kuzungumzia
"Kwa sasa nawaza mchezo dhidi ya Ruvu Shooting. Huu ndio mchezo muhimu unaofuata kwenye ratiba yetu, habari ya ZESCO tutaizunguma baada ya mchezo huo"
"Pia siwezi kuzungumzia matokeo ya Simba kwa kuwa sikuona mchezo wao, sijui kilichotokea uwanjani," Zahera aliwaambia waandishi wa habari waliotaka atoe maoni yake baada ya Simba kutolewa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa
ADVERTISE HERE