Jana Metacha Mnata alikuwa shujaa wa mchezo akiisaidia Yanga kuondoka na ushindi muhimu wa bao 1-0 ugenini na kufanikiwa kutinga raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Pamoja na kudaka mkwaju wa penati kwenye dakika ya 64, Metacha alikuwa bora sana, akiifanya kazi yake ya ulinzi wa goli pamoja na kuzungumza na walinzi wake wakati wote
Katika nafasi ambayo wanayanga watapata usingizi msimu huu ni langoni
Kwa hakika kocha Mwinyi Zahera anastahili pongezi kwa mapendekezo ya usajili wa walinda lango Metacha na Farouk Shikalo
Kwa kiwango anaendelea kuonyesha Metacha, bila shaka Yanga inaweza isiwe na kipa namba moja, wote watatumika kulingana na mahitaji ya mechi
Pia itakuwa nafasi kwa Ramadhani Kabwili kujiimarisha na kupata uzoefu zaidi kutoka kwa walinda lango hao
Timu sasa ina magolikipa bora, huku pia ikiwa na safu ya ulinzi bora
Hii Yanga ya mwaka huu kuifunga itabidi ufanye kazi kwelikweli..!