Jana baada ya mazoezi ya asubuhi, kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera aliwapa ruhusu wachezaji kuvinjari jiji la Gaborone
Jioni kikosi kiliendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya Township Rollers ambao utapigwa kesho
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela ambaye ndiye kiongozi wa msafara, amesema kikosi kiko tayari kuwakabili Rollers
"Kikosi kinaonyesha mabadiliko makubwa hasa safu ya ushambuliaji. Kesho (leo) tutafanya mazoezi katika uwanja wa Taifa, Kikubwa tuna jipanga ipasavyo tunatumia nguvu zetu zote kuhakikisha tunapata matokeo," amesema
Wakati Yanga ikijifua hapo Gaborone, wenyeji wao Township Rollers wanafanyia maandalizi yao nje ya mji
ADVERTISE HERE